(baadhi ya wafanyabiashara wa eneneo lilobomolewa wakiwa na sintofahamu)
Bomoa bomoa ya waliojenga maeneo ambayo yamekatazwa na serikali imeanza kwa ghafla eneo la mwenge hali ambayo ilmeleta mtafaruku kwa wamiliki wa maeneo hayo ambayo kwa asilimia 100 ni maeneo yalopangishwa kwa wafanyabiashara,,,
(baadhi ya eneo liliobomolewa)
Waboamoaji hao walitinga na matingatinga hayo na kuanza kubomoa kwa fujo iliyopelekea baadhi ya bidhaa kufunikwa na mabaki ya matofali,mabati,mbao pamoja na udongo uliotokana na ubomoaji huo.hali iliyopelekea wamiliki wa maeneo hayo kupata shida kubwa na mateso katika kuokoa mali zao.
( pichan ni wafanyabiasha ndogondogo wa eneo hilo wakilinda mabak ya vitu)
Baadhi ya wafanyabiashara hao wameilalamikia serikali kwa kitendo cha kuvamia ghafla eneo hilo bila taarifa maalumu ya kuwapa wajiandae kutoka eneo husika kabla ya kubomoa.
"fikiria mpaka sasa hatujalipwa sisi ambao tuna frem za biashara af wanatuvamia tu wakati tulishajenga majengo yetu kabla ya matangazo yao ya kutaka kubomoa"alisikika mama neema ambaye ni mmoja wa waliokutwa na shida hiyo..nae Juma Khamis ambae ana steshenali eneo hilo alisema haya,,nanukuu "kwa nini aanze na sisi walalahoi asianze na hao MAFISADI PAPA anaosema atajenga mahakama yao?au anaogopa kuanza kuvunja kwa vigogo wenzie??aantaka tuingie mtaan tuanze kuua??mi naona hataki vijana tufanye kazi anata tudhurure alimalizia jama huyo kwa jazba."mwisho wa kunukuu...
wazo langu naona serikali ingeweka wazi kuhusu ubomoaji huu na ingetoa taarifa siku 3 kabla ya ubomoaji ili wahusika waweze ondoa mali zao na kuzihifadhi vizuri,na ckuvamia tu wanaumiza wanachi
(wali nazi...)
No comments:
Post a Comment