Pages

Saturday, October 17, 2015

                                        (kocha msaidizi wa timu ya yanga Juma Mwambusi)



Inawezekana baadhi ya wadau walikuwa hawamfahamu sana Mwambusi unajua kwa nn?? huyu jamaa si mmoja kati ya makocha waongeaji sana kwenye vyombo vya habari, ila ki ukweli ana mafanikio mengine makubwa zaidi kwani ndiye aliyeiwezesha timu ya Mkoa wa Mbeya ‘Mapinduzi Stars’ kuchukua ubingwa wa Kombe la Taifa mara mbili tofauti, Pia wadau wa soka walikuwa hawamfahamu hadi pale alipoipandisha Mbeya City katika Ligi Kuu msimu wa 2013/14 na kuifanya iwe tishio kubwa kwenye msimu wake wa kwanza tu, ambapo timu hiyo ilifanikiwa kucheza kwa kiwango kikubwa na kumaliza ikiwa nafasi ya tatu ikiipikua Simba iliyoangukia nafasi ya nne.
     
  Mwambusi kwa sasa amejiunga na Yanga akienda kufanya kazi kama Kocha Msaidizi na imani ndoto zake za kwenda kushiriki michuano ya kimataifa zitatimia..nenda mjombaaa,,, najua utajifunza mbinu nyingi za kiuchezaji katika michuano hii mikubwa nafasi ambayo ingekua ngumu kuipata kama bado ungebaki MBEYA CITY. Na am sure daraja lako litapanda kwa kufanya kazi na kocha hans........

No comments:

Post a Comment