Pages

Wednesday, June 19, 2013

RIHANA AMSHINDA JUSIN BIEBER KWA VIDEO ZAKE KUTAZAMWA ZAIDI MTANDAONI.

Robin Rihanna Fenty a.k.a Rihanna anazidi kung'aa kwenye
ulimwengu wa RnB mwaka huu, baada ya kuvunja record kwenye billboard
charts sasa amehamia kwenye vichupa
vyake 77 vilivyo You Tube ambapo ameichukua nafasi ya kwanza kwa kuwa na
watazamaji wengi zaidi ya waimbaji wenzake na kumfunika Justin Bieber aliyekuwa
ameishikilia nafasi hiyo.

Video za Rihanna zimefikisha jumla ya watazamaji billion
3.788 hadi kufikia jana jumanne(june 18) wakati Justin Bieber mwenye vichupa 79
vya kutazamwa amezidiwa na Rihanna watazamaji million 2.
Nafasi ya tatu inashikiliwa na Mkorea  mzee wa Gangnam ambae amepata jumla ya watazamaji billion 3.1 wa video zake zote, nafasi
ya nne imeenda kwa rapper asiyechuja Eminem mwenye jumla ya watazamaji billion
2.4,na nyingine imetua kwa mwanadada Lady gaga ambayo ni idadi ya
billion 2.3, na nafasi ya tano imeenda kwa Ray C wa mtoni ambae kiuno chake
hakiongopi Shakira ambae amepata jumla ya watazamaji billion 2.
Kwa upande wa mtandao wa kijamii wa Twitter bado justin
Bieber ndiye mfalme wa Twitter kwa kuwa na followers wengi zaidi ya wasanii
wenzake. Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa msanii wa kwanza kwa
walio hai kufikisha idadi ya followers million 40 na kumfunika mkongwe Lady
Gaga

No comments:

Post a Comment