Pages

Friday, April 19, 2013

VIDEO MPYA YA PSY(GENTELMAN) INASIKU CHACHE TU LAKINI VIEWZ ZAIDI YA 58 MILIONI

Mwanamuziki kutoka Korea ya Kusini ,Psy, anaeshikilia rekodi ya video iliyotazamwa zaidi kwa wimbo wake "Gangnam Style", sasa amerudi na kutoka na video nyingine ya wimbo unaoitwa "Gentleman". watu wengi wamekua wakizungumza kuwa Psy hawezi kuja kutoka na video nyingine ambayo itaweza kuipita Gangnam style,
lakini yeye mwenyewe alipokuwa akizungumza na CNN leo hii amesema hatarajii kuja kupita mafanikio ya video hiyo ya kwanza lakini akasema "wengi wameiongelea video hiyo ya gangnam style kama ni phenomena lakini hatuwezi kuelezea phenomena ni nini."
hata alipoongelea kufanikiwa kwake na kazi yake hiyo ya Gangnama alisema "sikuwa na fomula yoyote ya kunifikisha hapa nilipo so chochote kinawezekana"

kwa sasa video ya wimbo wake mpya "gentleman" umefikisha watazamaji 58,474,746 ndani ya siku 2 tangu ilipoingia kwenye youtube siku ya tarehe 13 april

No comments:

Post a Comment